Mabadiliko ya tabia nchi yasabisha viwango vya juu vya joto
31 Desemba 2024Matangazo
Kwa mujibu wa wataalamu wa Umoja wa Mataifa ni kwamba mwaka huu ulizidi ule kwa nyuzijoto 0.3. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres alizungumzia "muongo wa joto kali".
Guterres alionya kuwa ifikapo mwaka wa 2025, nchi zitalazimika kupunguza kwa kiasi kikubwa utoaji wa hewa chafu na kufanya zaidi katika mpito wa nishati mbadala.
Kulingana na shirika la WMO, gesi chafu katika anga zinazohusika na ongezeko la joto zinaendelea kupanda hadi viwango vipya vya rekodi.