Majengo ya makumbusho yaliosanifiwa kisasa
Makumbusho ya muundo mpya. Nchi, taasisi au kampuni humudu anasa za majengo ya miundo ya kipekee yaliosanifiwa na wasanifu maarufu duniani. Hii hapa ni sanaa ya majumba hayo ya makumbusho
Vivutio vya Ujerumani
Makumbusho ya Kiyahudi ya Berlin inaonyesha historia ya miaka 2000 ya Wayahudi wa Ujerumani, mabonde na milima katika uhusiano kati ya Wayahudi na wasio Wayahudi nchini Ujeurumani. Ina maonyesho ya kudumu, hifadhi ya nyaraka, kituo cha mafunzo cha Rafael Roth na vifaa vya ufatifi. Idara hizi zote zinawakilisha utamaduni wa Kiyahudi na historia ya Wayahudi wa Ujerumani.
Ujenzi wa Makumbusho ya Folkwang Essen
Makumbusho hayo yamejengwa na David Chipperfield mwaka 2010. Jumba hilo lina sehehu kubwa ya wazi na kwa kutumia dirisha kubwa la kioo linalopitisha mwangaza mwingi. Hiyo ni alama ya uwazi na uhuru. Lakini pia ametumia baadhi ya sanana za kijapani katika ujenzi wa jumba hilo.
MAXXI: Makumbusho ya taifa ya sanaa za kisasa za karne ya 21
Kazi za Zaha Hadid kila siku huwa ghali na za kipee na zinahitaji kutazamwa kwa jicho pana. Kwahiyo makumbusho ya sanaa za kisasa yaliopo Rome pia yamo katika sifa hizo. Mwaka 2009 makumbusho hayo yalifunguliwa kwa dansi ya sanaa ya kisasa kutoka kampuni ya Sasha Waltz.
Mwonekano wa Wakfu wa Louis Vuitton
Jumba hili lilisanifiwa na msanifu majengo mwenye asili ya Canada na Marekani Frank Gehry, katika bustani ya Bois de Boulogne mjini Paris Oktoba 17, 2014. Jengo hilo linalochukuwa muundo wa boti inayoelea katika miti ya bustani ya Boise de Boulogne, lina matanga 12 ya birauli, na ni sehemu ya utamaduni wa muda mrefu wa uanifu wa birauli kama vile Grand Palace.
Makumbusho ya Musee des Confluences Lyon
Kundi la Coop Himmelblau kutoka Vienna ndio lililojenga jengo hili la kituo cha sayansi na makumbusho ya antropolijia mjini Lyon Ufaransa. Lilifunguliwa rasmi Disemba 2014. Mara nyingi kazi za kundi la Himmelblau kuendeleza ndoto, maswala ya kimsingi ya jamii kufahamu wakati na sehemu na uelewa wa dunia.
Jumba la sanaa la Kanada Edmonton
Nyumba la sanaa la Kanada lililoko Alberta katika jimbo la Edmonton.
Makumbusho ya Kanada Royal Toronto
Makumbusho ya kifalme ya Kanada ya Ontario mjini Toronto.
Makumbusho ya sanaa mjini Milwaukee Marekani
Makumbusho ya sanaa mjini Milwaukee Marekani
Makumbusho bioanuwai ya Panama
Muonekano wa makumbusho ya bioanuwai mjini Panama City wakati wa kuzinduliwa kwake Septemba 30,2014. Makumbusho hiyo inaonyesha mabadiliko ya shingo ya Panama, mimea na wanyama wake, na ndiyo kazi ya kwanza ya msanifu majengo wa Canada frank Gehry katika bara la Amerika Kusini.
Makumbusho ya sanaa za kisasa mjini Rio de Janeiro
Makumbusho ya sanaa za kisasa mjini Rio de Janeiro
Makumbusho ya sanaa ya sayansi Singapore
Muonekano wa nje wa makubusho ya Sanaa ya Sayansi ilioko Matina Bay Sands, Singapore. Makumbosho hiyo ilisanifiwa na msanifu mashuhuri Moshe Safdie.
Makumbusho ya sanaa za Kiisilamu Doha, Qatar
Makumbusho ya sanaa za Kiisilamu Doha, Qatar inavyoonekana nyakati za asubuhi.