1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mengine yote yaliwezekana

31 Agosti 2016

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel. alitoa kauli ambayo sasa imekuwa maarufu, aliposema kuwa Ujerumani itaweza kuwamudu wakimbizi. Maoni tafauti yametolewa juu ya kauli hiyo

https://p.dw.com/p/1Jsvo
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel
Kansela wa Ujerumani Angela MerkelPicha: picture-alliance/dpa/R. Jensen

Na hakika ataweza hata ikiwa Kansela Merkel mwenyewe anahisi kubanwa juu ya msemo wake "tutaweza." Itawezekana kama jinsi ilivyowezekana katika mambo mengine yote.

Kwa mfano iliwezekana kuwasajili wakimbizi wapatao Milioni moja hata kama ilionekana kwa miezi kadhaa kana kwamba isingeliwezekana. Katika hilo tumejifunza kwamba tumeyapitisha makadirio ya uwezo wetu kuhusu umahiri wetu katika maanadalizi.

Lakini baada ya vurumai kubwa iliyotokea katika kipindi cha baridi,idara kuu ya Ujerumani inayoshughulikia wakimbizi na wahamiaji sasa ipo imara na maalfu ya wafanyakazi kufanikisha mambo.Mkuu wa idara hiyo amesema mambo yatakamilika hadi mwishoni mwa mwaka huu.

Wakimbizi wapatiwa makaazi ya kudumu

Idadi kubwa ya wakimbizi wameshaondoka kwenye sehemu za dharura na wametawanywa kwenye miji na sehemu nyingine mbalimbali.

Serikali kuu, za majimbo na za mitaa zilikubaliana mnamo mwezi wa Julai kutenga kiasi cha Euro Bilioni 7 kwa ajili ya kuwahudumia wakimbizi. Kwa jumla, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu serikali ya Ujerumani ilipata ziada ya Euro zaidi ya Bilioni 18. Na kwa hivyo kiuchumi itakuwa rahisi kufanikisha malengo.

Mwandishi wa maoni Dagmar Engel
Mwandishi wa maoni Dagmar EngelPicha: DW/S. Eichberg

Katika kipindi cha miezi 12 iliyopita tulijifunza mambo juu na chini.Tuliweza kuliona wimbi la ajabu la watu waliokuwa tayari kutoa msaada endelevu, lakini wakati huo huo tumekuwa tayari kukiri kwamba hakuna binaadamu aliekamilika.

Tumeweza kutambua katika nchi hii tajiri na ya utulivu mkubwa, pia wapo watu wengi wenye hofu, na pia wapo wale wanaoitumia hofu hiyo kwa shabaha zao za kisiasa. Hata hivyo sasa tunacho kifua cha kukabiliana na mvutano huo licha ya ukweli kwamba Wajerumani kwa jumla ni watu wanaoepuka mijadala.

Ujerumani haijawahi kukabiliwa na mjadala mkali kama huo:tunu ilioje: Demokrasia inahitaji malumbano ili kuweza kufikia maamuzi. Tamefanikiwa kuondoka kwenye tabia ya muda mrefu ya kujificha katika upole wa kufikia mwafaka- huo ndiyo msingi wa kukomaa.

Tumeweza kuondokana na mawazo juu ya utaifa wa kijerumani japo tangu mwanzo hicho kilikuwa kisasili. Wakati wote wamekuwapo wahamiaji nchini Ujerumani wa namna mbalimbali,tango mwanzoni kabisa.

Historia ndiyo itakayotoa hukumu juu ya sera ya wakimbizi ya Ujerumani.Katika hukumu hiyo itatamkwa kwamba Wajerumani walikuwa na ujasiri wa kuwasaidia wakimbizi waliokuwamo katika masahibu, bila ya kuwa na hofu ya kuhusiana nao, na licha ya matatizo na ugumu wote. Wajerumani wanaitumia fursa:mwaka uliopita walianza kuufungua ukurasa wa historia ya mafanikio.Na hakika wamefanikiwa.

Mwandishi:Engel,Dagmar

Mfasiri:Mtullya abdu.

Mhariri:Iddi Ssessanga