Mapambano ya wanawake wenye ulemavu kukabili maisha
Ambia Hirsi15 Januari 2016
Mila zilizomuweka mtu mwenye ulemavu kwenye kundi la wale waliokosa fursa na watu wa pembeni inamuumiza zaidi mwanamke, ambaye tangu hapo huwa ameshawekwa kwenye makundi hayo katika jamii ambazo zinafuata mila hizo potofu, lakini kuna wanawake wengi wenye ulemavu ambao wameonesha ujasiri wa hali ya juu sio tu katika kuuvunja mduara huu wa papo kwa papo wa udhalilishaji, lakini pia kujiimarisha.