Marekani yaionya China dhidi ya ushindi wa Urusi, Ukraine
10 Aprili 2024Matangazo
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayehusika na Asia, Kurt Campbell, amesema kwa nchi yake, suala la kudumisha amani na utulivu barani Ulaya ni mojawapo ya majukumu muhimu ya kihistoria.
Wakati huu Moscow inaporejesha mashambulizi yake dhidi ya Ukraine huku kukiwa na mkwamo wa kuidhinishwa kwa msaada wa kijeshi kwenye Bunge la Marekani, Campbell ameonya kwamba mafanikio ya Urusi nchini Ukraine yanaweza kuchafuwa mizani ya madaraka kwa kiwango ambacho hakikubaliki.
Marekani imekuwa ikitishia kuiwekea vikwazo Beijing ikiwa itachukuwa hatua za kuisaidia Urusi.