Marekani yasema Urusi iliidugua kimakosa ndege ya Azerbaijan
28 Desemba 2024Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la MSNBC ikinukuu vyanzo viwili vya jeshi la Marekani. Ndege hiyo ilianguka Kazakhstan Jumatano, na dalili za awali zinaonyesha ililengwa na mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi.
Waziri wa Azerbaijan, Rashan Nabiyev, alirejelea ushahidi wa wataalamu na maelezo ya manusura kuthibitisha madai hayo.
Soma pia: Wataalamu wa anga wasema mifumo ya Urusi huenda iliiangusha ndege ya Azerbaijan
Taarifa za wataalamu wa anga zinaeleza kuwa mifumo ya Urusi ilijibu shambulio la Ukraine, na kuongeza shinikizo kwa Urusi, ambayo inadai kulikuwa na shambulio la droni karibu na eneo ambako ndege hiyo ilikuwa ikielekea kutua.
Msemaji wa Baraza la Usalama la White House, John Kirby, alithibitisha uwepo wa ushahidi wa awali lakini akakataa kutoa maelezo zaidi kutokana na uchunguzi unaoendelea.