Marufuku ya kutotoka nje yaondolewa mjini Damascus, Syria
12 Desemba 2024Siku ya Jumatano, mkuu wa muungano wa makundi ya upinzani ya Syria unaoongozwa na kundi la Hayat Tahrir al-Sham Ahmed al-Sharaa ambaye awali alijulikana kama Abu Mohamed al-Joulani amesema hawatakuwa na huruma katika kuwasaka wale wote waliowatesa watu wa Syria.
al-Sharaa ameongeza kuwa wale wote waliohusika katika kuwatesa na kuwauwa wafungwa hawatasamehewa na akazihimiza nchi za kigeni kuwarejesha nchini humo wahalifu waliotorokea katika miji yao.
Zaidi ya wafungwa 30,000 waliuawa nchini Syria kati ya mwaka 2011 na 2018
Wanaharakati wa haki za binadamu wanakadiria kwamba katika gereza maarufu la Sednaya pekee nchini Syria, zaidi ya wafungwa 30,000 waliuawa au kufa baada ya kuteswa, kunyimwa huduma ya matibabu au kutokana na njaa kati ya mwaka 2011 na 2018.
Chama cha Baath kinachoongozwa na Al-Assad chasimamisha shughuli zake kwa muda
Chama cha Baath kinachoongozwa na Al-Assad, kimetangaza kusimamishwa kwa muda kwa shughuli zake.
Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya chama hicho jana Jumatano ilisema shughuli zake zitasimamishwa hadi itakapotangazwa tena na kuongeza kuwa chama hicho kitakabidhi vitu vyote, magari na silaha walizo nazo kwa wizara ya mambo ya ndani.
Israel yakanusha vikosi vyake kuingia Syria
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa mali na fedha zote za chama zimewekwa chini ya usimamizi wa wizara ya fedha pamoja na ile ya sheria na mapato yake yanawekwa katika Benki Kuu ya Syria kutumika na serikali ya sasa kwa mujibu wa sheria .
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Damascus kufunguliwa tena
Katika hatua nyingine, Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Damascus unaweza kufunguliwa tena siku ya Jumapili. Haya ni kulingana na chanzo cha wizara ya uchukuzi kilicholiarifu shirika la habari la dpa.
Chanzo hicho kilichozungumza kwa sharti la kutotambulishwa, kimesema uwanja huo wa ndege ulikabiliwa na wizi na kuharibiwa vifaa vyake .
Chanzo hicho kimeongeza kuwa kazi ya marekebisho ilikuwa ikiendelea katika uwanja huo lakini baadhi ya vifaa havipatikani nchi humo hali inayochangia marekebisho hayo kuchukuwa muda.
Wanamgambo wa Kikurdi kuondoka mjini Manbij
Wanamgambo wa Kikurdi wa Syria ambao wanaungwa mkono na Marekani, wamesema wataondoka katika mji wa kaskazini mwa Syria wa Manbij na kuachia vikosi vya upinzani vinavyoungwa mkono na Uturuki chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na Marekani.
Iran yazishutumu Israel, Marekani kwa anguko la Assad
Wapiganaji hao wa Kikurdi walikuwa wameuteka mji huo kutoka kwa wanamgambo wa itikadi kali wanaojiita dola la kiislamu IS mnamo mwaka 2016.
Shirika la Uangalizi wa Haki za Binadamu la Syria pia limethibitisha kuwa wanamgambo wa kundi la wapiganaji la Syrian National Army (SNA) wanaoungwa mkono na Uturuki wamechukuwa udhibiti wa Manbij.
Qatar kufungua tena ubalozi wake Syria
Qatar imesema itafungua tena ubalozi wake nchini Syria baada ya zaidi ya miaka 13.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Majed al-Ansari, amesema nchi hiyo inakamilisha mipango inayohitajika.