Umetimia mwaka mmoja tangu Urusi ilipoingia katika mgogoro wa Syria ambapo kwa mujibu wa waangalizi huru nchi hiyo imesababisha vifo vya watu zaidi ya elfu tisa. Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesisitiza kwamba katu hajabadili msimamo wake kuhusu sera ya wahamiaji. Na Pakistan imeutolea wito Umoja wa Mataifa kuingilia kati mvutano unaozidi kuenea baina yake na India juu ya eneo la Kashmir.