Merkel: "Tuko imara kuliko ugaidi"
31 Desemba 2016Mwaka 2016 unakaribia kumalizika , na mwaka 2017 unakaribia kuingia nchini Ujerumani. Katika hotuba yake ya mwaka mpya , kansela Angela Merkel alisema kwamba miezi 12 iliyopita "ilikuwa mtihani mkubwa kwetu katika njia nyingi." Miongoni mwa hizo , ugaidi wa itikadi kali ya Waislamu , "bisha shaka " ndio " mtihani mkubwa mgumu." Nchi ilishuhudia mlolongo wa mashambulizi kwa mwaka mzima: Mjini Würzburg, Ansbach na hivi karibuni kabisa , Berlin.
watu 12 waliuwawa wakati Anis Amri alipoendesha lori katika kundi la watu katika soko la krismass katika mji mkuu wa Ujerumani Berlin Desemba 19. Mtunisia huyo mwenye umri wa miaka 23 alikuja Ujerumani kama mkimbizi.
Ni "kitu kichungu - na kisichopendeza," alisema kansela , wakati mashambulizi ya kigaidi yanafanywa na watu "ambao wamekuja hususan kutafuta hifadhi , mahali salama na tena wamepata msaada." Vitendo hivi "vinabeza" kuwapo tayari kwa Wajerumani kutoa msaada , na pia kwa wale watu " ambao wanahitaji kweli msaada na wanastahili ulinzi."
Kuwapo na nia thabiti
Kama kawaida , majonzi kuhusiana na waliouwawa na waliojeruhiwa ni makubwa. Hii ilionekana katika hotuba ya Merkel. Katikati ya maafa kama hayo , Merkel alitoa wito wa kujiamini "katika mtazamo imara wa kusimama imara dhidi ya dunia ya chuki ya magaidi kwa ubinadamu wetu na mshikamano."
Kwa hakika , kansela na kiongozi wa chama cha kihafidhina cha Christian Democratic Union CDU, wamethibitisha msimamo wake kuhusiana na sera ya wakimbizi katika ujumbe wake kwa ajili ya mwaka mpya. "Na wakati tunakabiliwa na picha za mji uliopigwa mabomu wa Aleppo nchini Syria , tunasisitiza kwamba ni muhimu kiasi8 gani na muhimu kwa nchi yetu kuwachukua wale ambao kwa kweli wanahitaji msaada wa ulinzi, na kuwasaidia kuweza kujumuika hapa."
Kwa kansela , magaidi wanaishi katika "dunia iliyojaa chuki" na utawala wa sheria na demokrasia vinakwenda kinyume na hivyo. "Tuko imara wakati tutakapojiunga pamoja. Nchi yetu ni imara," alisema, na kuongeza kwamba taifa ni lazima pia lipambane na ugaidi ili kuweza kuhakikisha "usalama na uhuru" kwa raia wake. "Katika mwaka ujao , kama itakuwa lazima, serikali ya Ujerumani haraka itaanzisha na kuidhinisha sheria ya ziada na hatua za kisera," alisema Merkel.
Kuiokoa demokrasia na watu
Kansela ameelezea nia yake ya kuwa na umoja zaidi na kuimarisha demokrasia katika mwaka mpya. Watu wengi , alisema , watauhusisha mwaka 2016 na hisia kwamba dunia ilipinduliwa chini juu. Mafanikio kama Umoja wa ulaya na demokrasia ya bunge vilipata changamoto kwasababu vionekana kutojihusisha na maslahi ya raia.
"Lakini hii ni picha potofu," alisema Merkel . Ndio , Ulaya inaburuza miguu , alisema Merkel, "lakini sisi Wajerumani hatupaswi kuwa na mwelekeo ambao tunaamini kwamba kila taifa kuelekea katika njia yake kutaleta mafanikio ya baadaye.
Mwezi Septemba 2017 , Ujerumani itafanya uchaguzi mkuu. Merkel pia alidokeza hilo katika hotuba yake ya mwaka mpya. Demokrasia ya bunge inahitaji "upinzani na ukosoaji," lakini hali hiyo inapaswa kuwa ya amani na kuheshimiana.
"Nina nia ya kushiriki katika hatua za kisiasa ambazo zitashuhudia mijadala ya amani miongoni mwa raia wa kidemokrasia ambao kamwe hawasahau heshima kubwa iliyopo kuhudumia demokrasia yetu na watu wake," alisema.
Mwandishi: Sabine Kinkartz (dr) Sekione Kitojo
Mhariri: Isaac Gamba