TeknolojiaMarekani
Mtandao wa TikTok wazimwa Marekani
19 Januari 2025Matangazo
Haya yamejiri kabla ya sheria itakayoanza kutumika Jumapili inayohitaji kuzimwa kwa jukwaa hilo linalotumiwa na takriban Wamarekani milioni 170.
Kwa mujibu wa chapisho lililowekwa na Tiktok, Rais mteule Donald Trump, amesema kuna "uwezekano" wa kuahirisha kwa siku 90 marufuku hiyo mara baada ya kuchukua madaraka siku ya Jumatatu.
Soma pia: Venezuela yautoza faini ya dola milioni 10 mtandao wa TikTok
Hata ikiwa ni ya muda mfupi, kuzimwa kwa TikTok, inayomilikiwa na kampuni ya teknolojia ya China ByteDance , kunatarajiwa kuwa na athari kubwa katika uhusiano wa Marekani na China, siasa za ndani za Marekani, kijamii soko la vyombo vya habari na mamilioni ya Wamarekani ambao wanategemea mtandao huo kiuchumi na kiutamaduni.