NAIROBI: Wswaada wa viti 50 kwa wanawake washindwa bungeni
16 Agosti 2007Matangazo
Mswaada uliowasilishwa bungeni kutaka wanawake nchini Kenya wapewe nafasi maalum 50 za uwakilishi bungeni umeshindwa.
Kushindwa kwa mswaada huo kulisabishwa na kutokuwepo idadi ya kutosha ya wabunge kuujadili na hivyo kumlazimu spika wa bunge bwana Francis Ole Kaparo kuutupilia mbali mswaada huo.
Ni wabunge 95 pekee waliohudhuria kikao ili hali wanahitajika takriban wabunge 145 kuweza kujadili na kupitisha mswaada.
Miswaada mingine iliyoshindwa ni pamoja na ule wa kuongeza idadi ya maeneo bunge nchini Kenya na juu ya kubadilishwa kifungu nambari 33 cha katiba za Kenya.