Benjamin Netanyahu anasafiri leo kwenda Ujerumani
15 Machi 2023Netanyahu atakutana na Kansela Olaf Scholz na Rais wa Shirikisho Frank-Walter Steinmeier mjini Berlin hapo kesho.
Ziara hiyo inagubikwa na mzozo mkali nchini Israel kuhusu mageuzi tata ya idara ya mahakama ambayo yanasukumwa na serikali ya Netanyahu ya muungano ya mrengo wa kulia yenye misimamo mikali ya kidini.
Wapinzani wa mageuzi hayo wanatarajiwa kujaribu kumzuia Netanyahu kuondoka Israel kwa kuweka vizuizi barabarani.
Soma pia:Israel yazindua mpango wa mabadiliko ya sheria
Maandamano pia yanatarajiwa mjini Berlin kesho, na ziara ya Netanyahu itaambatana na operesheni kubwa ya polisi.
Kwa mujibu wa chama cha polisi, zaidi ya maafisa wa polisi 3,000 watawekwa mitaani kuanzia leo hadi Ijumaa asubuhi.
Ulinzi mkali umepangwa wakati Netanyahu atakapokuwa Berlin, huku barabara nyingi zikitarajiwa kufungwa.
Mazungumzo ya Netanyahu na Scholz yanatarajiwa kuangazia ushirikiano wa pande mbili, na masuala ya usalama wa kimataifa na kikanda.