1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Ban Ki-Moon aapishwa.

15 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjD

Kiongozi mpya wa umoja wa mataifa ameapishwa katika sherehe iliyofanyika mjini New York. Raia wa Korea ya kusini mwenye umri wa miaka 62 Ban Ki-Moon ameahidi kuwa kama mjenzi wa daraja na kuiongoza taasisi hiyo ya dunia katika njia bora na yenye matumaini.

Ban anachukua wadhifa huo akiwa ni katibu mkuu wa nane hapo Januari mosi na kiongozi wa kwanza kutoka katika bara la Asia kushika wadhifa huo katika muda wa miaka 35. Baraza kuu la umoja wa mataifa hapo kabla lilimpongeza katibu mkuu anayeondoka madarakani Kofi Annan , huku mabalozi wakimsifu kwa kuuongoza umoja wa mataifa kupitia katika wakati wake wa matatizo ya mageuzi.