1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Norway kusaka suluhu ya mataifa mawili kwenye mzozo wa Gaza

13 Januari 2025

Norway imesema, mataifa kadhaa yatapeleka wajumbe wao nchini humo siku ya Jumatano kama sehemu ya muungano wa kimataifa unaolenga kutafuta suluhu ya pande mbili katika mzozo wa Israel na Palestina.

https://p.dw.com/p/4p7rh
Gaza | Dair_el-Balah akikumbatia mwili wa mtoto wake mchanga
Dair_el-Balah mkazi wa Gaza akiomboleza kifo cha mtoto wake mchanga aliembeba.Picha: Omar Ashtawy/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Waziri Mkuu wa mamlaka ya Palestina Mohammed Mustafa, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA Philippe Lazzarini, na mjumbe wa Umoja wa Mataifa wa Mashariki ya Kati Tor Wennesland ni miongoni mwa watakaohudhuria mkutano huo.

Utakuwa ni mkutano wa tatu wa Muungano wa Kimataifa wa Utekelezaji wa Suluhu ya Nchi Mbili, ambao kuundwa kwake kulitangazwa mwezi Septemba kando ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.

Soma pia:Makubaliano ya kusitisha vita Gaza yakaribia kufikiwa

Hata hivyo,  Wachambuzi wanasema uwezekano huo bado ni mgumu kufikiwa wakati ambapo Israel yenyewe haiungi mkono hatua hiyo.