1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama atembelea CIA

21 Aprili 2009

Obama aeleza kwanini akomesha kuteswa wafungwa.

https://p.dw.com/p/HbDd
Barack ObamaPicha: AP

Rais Barack Obama wa Marekani jana alitembelea Makao makuu ya Shirika la Ujasusi la Marekani -Central Inteligence Agency (CIA) mjini Washington na alipokewa huko na watumishi wake kwa shangwe. Ziara yake ilifuatia hatua yake ya wiki iliopita ya kufichua hadharani taarifa nyeti jipatia habari ni ya njia zinazotumiwa na wapelelezi wa shirika hilo kujipatia habari kutoka kwa wafungwa na watuhumiwa wa ugaidi .Miongoni mwa mitindo iliotumiwa na CIA kujipatia habari ni kuwatesa wafungwa kuhisi wanazama majini.

Takriban mtu hupata dhana kana kwamba, Barack Obama ni kipenzi cha kila mtu kila endapo.Pale rais Obama alipowatembelea hapo jana watumishi wa Idara ya Ujasusi ya Marekani CIA huko Langley,Washington ,alikaribishwa kwa shangwe na shamra shamra.Na hii licha ya kuwa mwishoni mwa wiki iliopita Obama alikosolewa vikali na mkurungenzi wa zamani wa Idara hiyo ya CIA Hayden .Hayden alimkosoa Obama kwamba kwa kuzichapisha hadharani taarifa za kumbukumbu za jinsi wafungwa wanavyoteswa amejitia pingu binafsi katika vita vya kupambana na ugaidi:

"Nahisi,taarifa hizo zilizofichuliwa ni za faida kubwa kwa maadui zetu."Alidai mkurugenzi huyo wa zamani wa shirika la ujasusi la CIA.

Rais Obama lakini haklujali ila kama hizo na anafuata mkondo wake ule ule n a jana alikwenda katika pori la simba kunguruma:

"Nimekomesha mbinu za kuwahoji watuhumiwa zilizoelezwa katika dafutari la kumbukumbu na nataka kuweka wazi kabisa kuwa nimefanya hivyo kwa sababu moja -nayo ni kuwa naamini Taifa letu lina nguvu na litakuwa na usalama zaidi ikiwa tutatumia kikamilifu nguvu zetu za kijeshi na desturi na maadili yetu . Pamoja pia na utawala wa kisheria."

Rais Obama akaendelea kusema:

" Najua naweza kuwategemea nanyi kutenda hivyo kabisa."

Rais Obama alitetea uamuzi wake kutowafikisha mahkamani watumishi wa shirika la ujasusi la Marekani (CIA) kwa mitindo hiyo waliotumia ya kuwahoji wafungwa na ya kutatanisha.Alisema hakuna kitu muhimu zaidi kama kuwalinda watumishi wa CIA wasitambuliwe ni akina nani.Na ndio maana ataendelea kuwakinga na kuhakikisha usalama wao.

Zaidi rais Obama aliwaambia wafanyakazi wa CIA:

"Kilichoifanya marekani kuwa dola la kipekee na kilichowafanya nyinyi watumishi wa kipekee, ni kuwa tunafuata desturi na maadili yetu hata ikiwa tunauumia kwa kufanya hivyo."

Rais Barack Obama alhamisi iliopita alifichua hadharani kumbukumbu za mbinu za kuwahoji wafungwa enzi za utawala wa mtangulizi wake-rais George Bush.miongoni mwa mbinu zilizotumika kuwahoji wafungwa kutoa habari ni kuwatesa kwa njia za kana kwamba wanazamishiwa majini,wakipigwa makofi usoni.Imefahamika pia watuhumiwa wa kuandaa ile njama ya Septemba 11,2001 kama Khalid Sheikh Mohammed aliteswa hapo mwaka 2003 mara 183 kwa njia hiyo kana kwamba anazamishwa majini.

mitindo kama hiyo ameamua rais barack Obama kuikomesha.

Mtayarishi: Ramadhan Ali

Mhariri: Muhammed Abdul-Rahman