Katika Utamaduni na Sanaa tunaangazia jamii ya Ogiek, watu wanaoishi msituni, wakiwinda, ukusanya matunda na kuvuna asali. Wakio Mbogho anaelezea juhudi za watu wa jamii hiyo kulinda misitu kwani wanashukiwa kuharibu mazingira na kutokana na shughuli zao za kiutamaduni za kutafuta chakula.