Orodha ya timu 16 za mwisho kukamilishwa
17 Juni 2019Nafasi nane za hatua ya 16 za mwisho bado zinagombaniwa katika mechi za leo za mwisho za makundi, na China wataangushana na Uhispania huku timu zote mbili zikirataji kufuzu kutoka Kundi B. Wote waliwapiku Afrika Kusini na kushindwa na mabingwa wa zamani Ujerumani, na kwa hiyo matokeo ya sare leo yatatosha kwa kila timu, ukizingatia kuwa timu nne bora zitakazomaliza katika nafasi ya tatu zitafuzu.
Ujerumani itahitaji tu pointi moja dhidi ya Afrika Kusini ili kuongoza Kundi B na hiyo kuepuka uwezekano wa kukutana na Marekani katika 16 za mwisho.
Ufaransa watavaana na Nigeria ambao wanalenga kupenya katika hatua ya makundi ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika miaka 20.
Mabingwa wa 1995 Norway wanalenga kutinga hatua ya mtoano watakapovaana na Korea Kusini