Palestina yaitaka jamii ya kimataifa kuitia kishindo Israel
15 Januari 2025Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Wapalestina, Mohammed Mustafa, amesema Jumuiya ya Kimataifa italazimika kuendelea kuishinikiza Israel baada ya kufikiwa makubaliano ya amani Gaza, ikubali kuundwa kwa dola la Wapalestina.
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa tatu wa muungano wa kimataifa kuhusu utekelezaji wa mpango wa kuundwa madola mawili Mashariki ya Kati, waziri mkuu huyo wa Palestina, amesema Israel inapaswa kuoneshwa kipi ni haki na kipi ni makosa.
Soma pia: Baerbock afanya mazungumzo na maafisa wa Israel, Ukingo wa Magharibi
Amewaambia waandishi wa habari mjini Oslo kwamba kutumiwa kwa kura ya turufu katika kuzuia amani na uundwaji wa dola la Wapalestina ni jambo ambalo haliwezi kukubalika tena. Wajumbe kutoka takriban mataifa 80 na mashirika wamekutana Oslo, Norway katika mkutano huo wa Kimataifa.