Puma: Alama ya sanaa katika kuponya majeraha ya kihistoria
Mohammed Khelef14 Januari 2016
Mchezo wa kuigiza wa Puma unaonesha kuwa pale hadithi mbili zinapokutana njiani – moja ikiikimbia jana yake na nyengine ikiikimbilia kesho yake – panakuwa na fursa ya kujihakiki upya sio tu kama fanani na hadhira, bali pia kama wahusika wa hadithi zenyewe, kama watenda na watendwa wa mifumo yetu ya kisiasa na kijamii.