Rais Joe Biden wa Marekani yuko ziarani nchini Angola
3 Desemba 2024Matangazo
Ziara hiyo inajikita kwenye suala la mradi mkubwa wa miundo mbinu ambao unataka kuupiku uwekezaji wa China.
Rais huyo wa Marekani anayejiandaa kuondoka madarakani mwezi Ujao, aliwasili jana usiku katika nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta kuanza ziara hiyo ya siku mbili ambapo atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake rais Joao Lourenco, mjini Luanda.
Rais Biden katika ziara ya siku mbili nchini Angola
Baadae Biden atazungumza katika makumbusho ya kitaifa ya Utumwa wakati kesho Jumatano, atasafiri kwenda bandari ya Lobito, kusini mwa Luanda.
Marekani inatarajia kukarabati barabara ya reli ya usafirishaji wa madini kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Zambia hadi bandari hiyo ya Lobito.