SiasaUrusi
Rais Putin awasili China kwa ziara rasmi
17 Oktoba 2023Matangazo
Mkutano huo ulioandaliwa na China unalenga kujadili maendeleo yaliyofikiwa na China katika miradi ya miundombinu kimataifa.
Xi na Putin wanatarajiwa pia kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati.
Hapo jana Putin alisema pendekezo la China kuhusu mazungumzo ya amani na Ukraine linaweza kuwa msingi wa makubaliano ya amani. Ni kulingana na mahojiano aliyoyafanya na Televisheni ya China, ambayo yalichapishwa na ikulu ya Kremlin jana.
Putin aliishutumu pia Ukraine kwa kutokuwa na nia ya kushiriki mazungumzo hayo ya amani.
Lakini mara kadhaa serikali ya Kyiv imekuwa ikitoa sharti la kuondoka kwanza kwa vikosi vya Urusi katika ardhi yake, kabla ya kuanza mchakato wowote wa mazungumzo.