1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Kenya aahidi kukomesha utekaji nyara

28 Desemba 2024

Rais wa Kenya William Ruto ameahidi kukomesha vitendo vya utekaji nyara, kufuatia visa vya hivi karibuni vya watu kutoweka ambavyo vimelaaniwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu, wanasheria na wanasiasa.

https://p.dw.com/p/4odsW
Kenia | Der kenianische Präsident William Ruto
Rais wa Kenya William Ruto akizungumza wakati wa mkutano na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer kando ya Kikao cha 79 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Septemba 25, 2024.Picha: LEON NEAL/POOL/AFP via Getty Images

Akizungumza na umati wa watu jana Ijumaa akiwa mjini Homa Bay magharibi mwa Kenya, Ruto aliahidi kukomesha utekaji nyara huo lakini pia akawaambia wazazi "kuwajibikia" kwa watoto wao. Vikosi vya usalama katika taifa hilo la Afrika Mashariki vimeshutumiwa kwa kuwashikilia watu kadhaa kinyume cha sheria tangu maandamano yaliyoongozwa na vijana dhidi ya serikali mwezi Juni na Julai. Matukio ya hivi karibuni yamehusisha hasa vijana ambao wamemkashifu Ruto mtandaoni, huku mashirika ya kutetea haki ya binadamu yakikanusha madai ya polisi kutohusika na kutaka hatua zichukuliwe.