SiasaAsia
Rais wa Korea Kusini atetea tangazo lake la amri ya kijeshi
12 Desemba 2024Matangazo
Akilihutubia taifa leo kwa njia ya televisheni, Yoon amesema hatua hiyo ilikuwa kwa ajili ya kulinda demokrasia ya nchi.
Rais huyo anachunguzwa kwa makosa ya jinai kwa tuhuma za uasi.
Yoon ameushutumu upinzani kwa kutaka kumuondoa madarakani, na ameapa kupambana hadi mwisho.
Rais huyo wa Korea Kusini amelielezea Bunge la Taifa kama jinamizi linaloharibu utaratibu wa kikatiba wa demokrasia ya kiliberali.
Saa chache baada ya Yoon kuitoa kauli hiyo, vyama sita vya upinzani vimewasilisha hoja mpya ya kumuondoa madarakani kiongozi huyo.
Wiki iliyopita chama hicho kilishindwa katika jaribio lake la kwanza, baada ya chama tawala kuzuia mchakato wa kura ya imani.