1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Rais Xi Jinping asifu uhusiano wa China na Indonesia

Hawa Bihoga
1 Aprili 2024

Rais wa China amesifu uhusiano wa taifa lake na Indonesia alipokutana na Rais mteule Subianto na kuweka mipango ya baadae ya amani wakati mivutano inaongezeka baina ya China na mataifa ya kusini mashariki mwa Asia.

https://p.dw.com/p/4eJrO
Rais wa China Xi Jinping
Rais wa China Xi JinpingPicha: Yao Dawei/Xinhua News Agency/picture alliance

Rais wa China Xi Jinping amemwambia Prabowo katika mazungumzo mjini Beijing kuwa mahusiano baina ya mataifa hayo ya Asia yameingia katika hatua mpya ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, yenye ushawishi wa kikanda na kimataifa na kwa ajili ya amani na maendeleo ya dunia.

Aidha Xi amemsisitizia rais mteule Prabowo ambae anatarajiwa kuapishwa mnamo mwezi Oktoba kuwa ufunguo wa uhusiano thabiti baina yao "utazingatia kuaminiana, uhuru wa kuchagua, kusaidiana pamoja na usawa na haki".

Soma pia: Prabowo Subianto ashinda uchaguzi wa urais Indonesia 

Prabowo anafanya ziara yake ya kwanza kwa mshirika mkuu wa kibiashara wa Jakarta tangu ushindi wake katika uchaguzi mwezi uliopita. 

China imewekeza mabilioni ya dola katika miradi mikubwa ya kimkakati nchini Indonesia ikiwamo reli ya mwendo kasi.