1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME.Mswaada utakaowalinda wapenzi wa jinsia sawa wapitishwa

9 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTk

Baraza la mawaziri la Italia limeidhinisha mswaada utakaowapa haki watu wa jinsia sawa wanaoishi pamoja.

Lakini wakati huo huo baraza hilo la mawaziri halikuruhusu ndoa za watu wa jinsia sawa.

Waziri wa usawa wa Italia Barbara Pollastrini amesema mswaada huo utawalinda watu hao juu ya haki zao za mirathi na afya.

Baraza la mawaziri limepitisha mswaada huo licha ya upinzani na lawama kutoka chama cha Christian Demokratik na kanisa katoliki.