AfyaRwanda
Rwanda yatangaza kumalizika kwa mripuko wa Marburg
20 Desemba 2024Matangazo
Rwanda imetangaza kumalizika kwa mripuko wa homa ya Marburg nchini humo. Hii ni baada ya kupona mgonjwa wa mwisho siku 42 zilizopita. Akizungumza katika kikao cha waandishí habari, Waziri wa Afya Sabin Nsanzimana amesema imekuwa safari ndefu lakini sasa imefikia mwisho. Amesema tangazo hilo limetolewa kwa kufuata muongozo wa Shirika la Afya Duniani - WHO.
Nchi hiyo ya Afrika Mashariki ilithibitisha visa vyake vya kwanza vya ugonjwa huo, homa kali ya kuvuja damu ambayo inaweza kusababisha kifo, miongoni mwa baadhi ya wagonjwa, katikati ya Septemba.
Iliriodhesha visa 66 vilivyothibitishwa, ambapo kulikuwa na vifo 15 na wagonjwa 51 wakapona. Hayo ni kwa mujibu wa wizara ya afya nchini Rwanda.