Senegal yasema inafunga kambi zote za kijeshi za kigeni
28 Desemba 2024Matangazo
Waziri Mkuu wa Senegal, Ousmane Sonko, ametangaza kufungwa kwa "kambi zote za kijeshi za kigeni," hatua inayolenga hasa wanajeshi wa Ufaransa, ambalo ndiyo taifa pekee la kigeni lenye kambi za kijeshi nchini humo.
Ingawa hakutoa muda maalum wa kuondoka kwa wanajeshi hao, tangazo hilo limekuja mwezi mmoja baada ya Rais Bassirou Diomaye Faye kusema kuwa hivi karibuni hakutakuwa na wanajeshi wa Ufaransa nchini Senegal.
Soma pia: Yafahamu mataifa mengine ya magharibi yenye vikosi vya kijeshi Afrika Magharibi
Ufaransa, iliyokumbwa na upinzani kutoka kwa viongozi wa Afrika kutokana na madai ya dharau na ubabe kuelekea Afrika, imetimuliwa kutoka mataifa ya Mali, Niger, na Burkina Faso, na tayari imeanza kukabidhi baadhi ya kambi zake nchini Chad.