Tarehe 8 Machi ulimwengu huadhimisha Siku ya Wanawake. Mwaka 2020 maadhimisho haya yamekwenda sambamba na miaka 25 ya maazimio ya Beijing pamoja na mkakati maalumu kuelekea haki na usawa wa kijinsia. Pamoja na harakati hizo, bado pengo ni kubwa kuanzia nafasi ya mwanamke nyumbani hadi ofisini. Lilian Mtono anakufahamisha jinsi wanawake wa Mexiko walivyoweka mgomo kuonyesha umuhimu wao.