1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haki ya kinga ya Ukimbizi Ulaya

5 Februari 2016

Wanawake wanaokabiliwa na kitisho cha kukeketwa wanaweza kuomba kinga ya ukimbizi katika nchi za Umoja wa Ulaya.Lakini hata katika nchi hizo hawako salama.Kwasababau mtindo huo unaaensdelezwa pia huku huku Ulaya.

https://p.dw.com/p/1HqG9
Kisu kinachotumiwa kumkeketa msichanaPicha: picture-alliance/dpa/Unicef/Holt

Visa vya ukeketaji vinashuhudiwa takriban kila siku katika kila pembe ya dunia.Na hasa katika pembe ya Afrika,Afrika Magharibi,Mashariki ya Kati na Asia,wanawake wanaangukia mhanga wa desturi hizo.Kwa mujibu wa shirika linalopigania haki za wanawake,Terre de Femmes,Somalia ndiyo inayoongoza orodha ya wanawake wanaokeketwa.Asili mia 98 ya wanawake wenye umri wa kati ya miaka 15 na 49 wamekeketwa katika nchi hiyo.Hata katika nchi jirani za Ethiopia na Sudan idadi ya wanaokeketwa ni kubwa-inapindukia asili mia 70.Shirika la afya la kimataifa WHO linakadiria wanawake wasiopungua milioni 150 wamekekletwa kote ulimwenguni.Kila mwaka wasichana milioni tatu wanaangukia mhanga wa desturi hizo.

Wanawake wanaokimbilia katika nchi za Umoja wa Ulaya ili kuepukana na balaa la ukeketaji, wanaweza kuomba kinga ya ukimbizi katika nchi hizo."Utaratibu wa kinga ya ukimbizi katika nchi za Ulaya unafuata muongozo wa makubaliano ya Geneva kuhusu wakimbizi.Wanawake wanaohofia wasije wakakeketwa wanaweza kupata kinga ya ukimbizi kwa msingi wa kuwa katika kundi fulani la jamii.Unaandamwa kwasababu wewe ni sehemu ya jamii fulani.Kwa hivyo ile hali kwamba unahofia usije ukakeketwa ni sawa na kuandamwa.Kwa hivyo inamaanisha wanawake wanaweza kupata kinga ya ukimbizi kwa msingi wa makubaliano ya Geneva."Anasema Sophie Forrez wa shirika la Ubeligiji linalotoa ushauri kuhusiana na masuala ya sheria-Intact.

Idara za uhamiaji barani Ulaya zinashughulikia kwa namna tofauti maombi ya kinga ya ukimbizi kwa wanaokabiliwa na kitisho cha kukeketwa

Wanawake wengi waliokimbia lakini hawajui chochote kuhusu kifungu hicho cha sheria,anasema kwa upande wake Linda Ederberg wa shirika la haki za wanawake-Terre des Femmes.Idara za uhamiaji katika nchi wanachama wa Umoja wa ulaya zinaweka wazi lakini "ikiwa kitendo cha ukeketwaji kimeshatendeka,hapo inamaanisha mtu hana sababu ya kuomba kinga ya ukimbizi.

Weibliche Genitalverstümmelung Girl Summit 2014 in London
Mkutano wa London ulioitishwa mwaka 2014 dhidi ya kukeketwa wasichanaPicha: picture-alliance/empics

Hadi wakati huu idara zinazohusika na masuala ya wahamiaji zimekuwa zikiyashughulikia maombi ya ukimbizi ya waliokeketwa au wanakabiliwa na kitisho cha kukeketwa,moja baada ya jengine.Waliokwisha keketwa,maombi yao mara nyingi hukataliwa,licha ya kwamba halmashauri kuu ya Umoja wa ulaya imeshatoa mwongozo thabiti kuhusu namna ya kuwashughulikia waliokeketwa.Umoja wa Ulaya unachunguza nchi gani hazikufuata mwongo huo mpaka sasa.

Juhudi za kuwaeleza wanawake wazijue haki zao zinaendelezwa

Lakini hata wanapokuwa Ulaya wanawake hao wanajikuta wakiandamwa na desturi hizo.Inakadiriwa sio tu watu laki tano waliokeketwa wanaishi katika nchi za Umoja wa ulaya,lakini pia wasichana na wanawake 180.000 wanaoishi Ulaya wanakabiliwa na hatari ya kukeketwa.

Äthiopien Kampagne gegen weibliche Genitalverstümmelung
Kampeni dhidi ya ukeketwaji nchini Ethiopia.Picha: DW/G. Tedla HG

Walter Lutschinger wa wakfu wa "Uwa la jangwani",shirika la kuwahudumia wahanga wa ukeketwaji kutoka Austria,ameunda mwaka 2013 hospitali inayoitwa Weltfried au Amani ya dunia mjini Berlin inayowashughulikia wahanga wa ukeketwaji.

Hospitali hiyo inakamata mstari wa mbele katika kuwashughulikia wahanga wa ukeketwaji.Shirika la Terre des Femmes linahimiza pia juhudi zifanywe katika daraja ya miji ili kuwafumbua macho wasichana na wanawake nini cha kufanya wakiona wanakabiliowa na kitisho cha ukeketwaji huku huku waliko.

Mwandishi: Krinninger,Theresa/Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Iddi Ssessanga