SINGAPORE: Wolfowitz asema benki ya dunia na Singapore zimeathiriwa
15 Septemba 2006Matangazo
Rais wa benki ya dunia, Paul Wolfowitz, amesema leo kwamba benki hiyo pamoja na Singapore zimeathiriwa kwa sheria kali dhidi ya watetezi waliotaka kuhudhuria mikutano ya kila mwaka ya shirika la fedha la kimataifa, IMF na benki ya dunia.
Watetezi waliokasirishwa na hatua ya Singapore kuwazuia wanaharakati 27 wasihudhurie mikutano hiyo, waliyagomea mazunguzo na kutoka nje ya mkutano.