STOCKHOLM : Mjerumani atapata Tuzo ya Nobel ya Fizikia
5 Oktoba 2005Matangazo
John Hall na Roy Glauber wa Marekani pamoja na Theodor Hänsch wa Ujerumani wameshinda tuzo ya Nobel ya Fizikia.
Hall na Hänsch wameshinda tuzo huyo kutokana na kazi yao ya kutengeneza chombo cha kuangalia kwa usahihi kabisa mpangilio maalum wa taswira zinazotokana na miali ya mnunurisho.
Akizungumza na Radio Deutsche Well Hänsch amesema anataraji tuzo hiyo itakuza wasifu wa fizikia nchini Ujerumani.
Tuzo hiyo ina thamani ya kama euro milioni 1 na laki 1.