Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema umoja huo, unahitaji Dola bilioni 4.4 za dharura kwa ajili ya kuyasaidia mataifa yenye njaa//Ikulu ya Marekani imechelewesha kutangaza amri mpya za rais za kuwazuia raia wa mataifa saba ya Kiislamu kuingia nchini humo//Urusi imeitaka Syria kuacha mashambulizi wakati wa duru mpya ya mazungumzo ya amani yanayoanza leo mjini Geneva, Uswisi