Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ahimiza amani na uvumilivu katika kuutafutia ufumbuzi mzozo wa Ukraine. Shirika la afya ulimwenguni WHO lazihimiza nchi tajiri kutoa haraka dola bilioni 16 kuudhibiti ugonjwa wa COVID-19. Na Waziri Mkuu wa Libya Abdulhamid al-Dbeibah anusurika jaribio la kumuua.