Makala ya Utamaduni na Sanaa inajikita katika tatizo wanalopata baadhi ya watu wanaoishi maeneo fulani ya Tanzania ama watu wa jamii fulani ambao katika mazungumzo huchanganya herufi "L" na "R". Utafiti unaonyesha kwamba lugha za asili hukiathiri Kiswahili kwa njia mbalimbali. Anuary Mkama anakueleza mengi zaidi katika kipindi chake.