Trump asema atakutana 'haraka sana' na Putin.
14 Januari 2025Hata hivyo, hakutoa muda mahsusi wa mkutano huo, ambao utakuwa wa kwanza kati ya viongozi wa nchi hizo mbili tangu Urusi ilipoivamia Ukraine mnamo Februari, mwaka 2022.
Alipoulizwa kuhusu mkakati wake wa kuvimaliza vita hivyo, Trump ameuambia mtandao wa Habari wa Newsmax kwamba, kuna mkakati mmoja tu na hilo litaegemea kwa Putin.
Soma pia: Trump na Putin kufanya mazungumzo kwa njia ya simu
Mike Waltz, ambaye ni mshauri mpya wa usalama wa taifa alieleza siku ya Jumapili kwamba anatarajia viongozi hao wawili - Putin na Trump, kuzungumza kwa njia ya simu katika siku au wiki chache zijazo.
Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwaacha mamilioni ya wengine bila maakazi rasmi na umesababisha pia mahusiano kuvunjika kati ya Moscow na mataifa ya Magharibi tangu mgogoro wa makombora wa Cuba wa mwaka 1962.