1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China na Irani zimesema Mashariki ya Kati si uwanja wa vita

28 Desemba 2024

Wanadiplomasia wakuu wa China na Iran leo hii wamekubaliana kwamba Mashariki ya Kati "si uwanja wa vita kwa mataifa makubwa" na haipaswi kuwa uwanja wa ushindani wa siasa za kilimwengu kwa mataifa ya nje ya eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4oeID
Libanon Journalistin berichtet
Mwandishi wa habari wa Lebanon katika kitongoji cha Tayouneh cha Beirut mnamo Desemba 02, 2024.Picha: ELIE BEKHAZI/ABAAD/AFP

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Beijing, Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi na mwenzake wa China Wang Yi walikubaliana kwamba "jumuiya ya kimataifa inapaswa kuheshimu mamlaka, usalama, utulivu, umoja na uadilifu wa eneo la nchi za Mashariki ya Kati. Washirika hao wawili wakuu wa kibiashara wameurejea tena wito wa kusitishwa kwa mapigano huko Gaza, kutekelezwa ipasavyo kwa usitishaji mapigano nchini Lebanon, na "uendelezaji jumuishi wa kukabiliana na ugaidi, maridhiano na michakato ya kibinaadamu nchini Syria" Mataifa yote mawaili,China na Iran, yalikuwa yakimuunga mkono rais aliyepinduliwa wa Syria Bashar al-Assad. Kiongozi mpya wa Syria, Ahmed al-Sharaa, ni mpinzani mkubwa wa Tehran.