Visiwani Comoro kuna kile kinachoitwa "harusi kubwa" au "ada" ama kwa kiingereza "the grand marriage." Ni utamaduni wa Wakomoro unaowafanya kutambulika kote duniani. Wanasema "ada" ni sawa na mauti, yaani ni lazima kila Mkomoro aipitie. Fahamu mengi zaidi katika "Utamaduni na Sanaa" na Saumu Mwasimba.