Uhuru afunga mpaka wa Kenya na Tanzania na Somalia
16 Mei 2020Matangazo
Katika amri aliyoitoa Jumamosi (16.05.2020) watu hawataruhusiwa kusafiri kuingia au kutoka Kenya kwenda Tanzania na Somalia, lakini mizigo itaruhusiwa. Hata hivyo katika amri hiyo itakayoanza kutekelezwa kuanzia Jumamosi saa sita usiku, rais Uhuru amesema madereva watatakiwa kupimwa kubaini kama wameambukizwa virusi vya corona. Watakaopatikana wameambukizwa hawataruhusiwa kuingia Kenya.
Akizungumza mjini Nairobi, rais Uhuru pia ameurefusha muda wa watu kutotoka nje kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi na moja alfajiri kwa siku 21. Kipindi kilichotangazwa awali kilikuwa kinakamilika leo.
Uhuru pia amerefusha hadi Juni 6 kufungwa kwa mipaka ya eneo la kibiashara la Nairobi, kaunti ya Mombasa, Kilifi, Kwale na Mandera.
(reuters)