1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani ilivyopokea ushindi wa Trump

Jane Nyingi
9 Novemba 2016

Ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi mkuu nchini Marekani umesalia mjadala mkubwa Ujerumani, huku kansela Angela Merkel akisema atabidi azingatie maadili ya pamoja ya kidemokrasia katika ushirikiano na Ujerumani

https://p.dw.com/p/2SQU1
Deutschland Reaktion US-Wahl - Bundeskanzlerin Angela Merkel
Picha: Reuters/A. Schmidt

Kansela huyo pia  alimkubusha  rais huyo mteule  wajibu alionao duniani baada ya kupigiwa kura kwa wingi na Wamarekani.Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin pindi baada ya John Donald Trump kutangazwa mshindi kansela Merkel alianza kwa kusema hivi “Nampongeza mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Marekani Donald Trump. Marekani ni taifa linaloheshimika na linalozingatia democrasia tangu zamani. Kampeini ya mwaka huu  ilikuwa ya aiana yake, na wakati mwingine ilikumbwa na makabiliano yaliyokuwa magumu kuvumiliwa.” Kansela Merkel amesema yuko tayari kwa ushirikiano wa karibu  na rais huyo mteule  chini ya misingi ya maadili ya mataifa yanayopakana na bahari ya Atlantic.Wakati wa mkutano huo Merkel alisisitiza kuhusu uhusiano wa karibu wa kihistoria kati ya Ujerumani na Marekani. Hata hivyo alimtaka Trump kuelewa anakabiliwa  na kibarua kigumu kutokana na Marekani kuwa taifa lenye uwezo mkubwa duniani linapokuja swala la kiuchumi na hata nguvu za kijeshi.

US-Präsidentschaftswahl 2016 - Sieg Donald Trump
Rais mteule wa Marekani Donald TrumpPicha: Reuters/M. Segar

Wakati wa kampeini zake Trump  alimtuhumu Merkel kutokana na kile alichokisema ni kuangamiza Ujerumani kutokana na sera yake ya milango wazi kwa wakimbizi, lakini baadae alimtaja kuwa  kiongozi anaye heshimika duniani. Nae waziri wa mambo ya nje  Frank-Walter Steinmeier  ameonya sera za kigeni za Marekani huenda zisiweze kutabirika  baada ya Trump; kuchaguliwa kwa wingi wa kura nchini Marekani. Steinmeier amesema anahofia hali hiyo huenda ikayafanya mambo kuwa magumu zaidi.“Wengi wetu tunatumai hakutakuwepo na mabadiliko makubwa ya sera za kigeni. Donald Trump alizungumzia hilo kwa kina wakati wa kampeini zake,sio tu kuhusu bara ulaya  lakini pia kuhusu Ujerumani.Nadhani itatubidi  katika siku za usoni kuzoea  sera za kigeni za Marekani  zisizotabirika, na lazima pia tukubali kuwa Marekani itafanya maamuzi kivyake.”

Florida Trump-Anhänger David Ramirez
Wafuasi wa Donald TrumpPicha: picture-alliance/ZUMAPRESS

Donald Trump  anataka kuijadili upya mikataba ya kibiashara ya Marekani ili kupunguza nakisi za biashara. Kwa mujibu wa Steinmeier,rais huyo  mteule  pia amechukua msimamo utakaohatarisha  uhusinao  kati taifa hilo na washirika wake wa karibu  bara Ulaya ,Asia na mashariki ya kati. Wakati wa kampeini zake Trump aliahidi kuanzisha uhusiano mzuri na Urusi, ambao ulivurugika chini ya utawala wa rais Barack Obama ,baada ya rais wa Urusi Vladmir Putin kuingilia vita vya Syria na vile vya Ukraine eneo la Krimea.

 

Mwandishi:Jane Nyingi/AFPE/AP
Mhariri:Yusuf Saumu