SiasaUrusi
Ujerumani na Urusi wafukuziana wanadiplomasia
23 Aprili 2023Matangazo
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi, Maria Zarakhova, amesema azma hiyo inafuatia hatua ya Ujerumani ya kuwaondoa watumishi wa ubalozi wake, lakini pia inalenga kupunguza idadi ya wafanyakazi katika ubalozi wa Ujerumani, mjini Moscow.
Afisa wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani amesema Berlin na Moscow zimekuwa zikifanya mawasiliano kuhusiana na idadi kamili ya uwakilishi katika wiki chache zilizopita kwa lengo la kupunguza uwepo wa maafisa wa kijasusi wa Urusi nchini humo.
Uhusiano kati ya Urusi na Ujerumani, ambayo ilikuwa mnunuzi mkubwa wa mafuta na gesi ya Urusi, umevurugika tangu Urusi ilipoivamia Ukraine mapema mwaka uliopita.