1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yajiandaa kuukaribisha mwaka mpya

Saleh Mwanamilongo
31 Desemba 2024

Sherehe kubwa zaidi ya mkesha wa mwaka mpya nchini Ujerumani huenda ikafanyika tena mbele ya lango la Brandenburg mjini Berlin, ambapo, kulingana na waandaaji, hadi watu 65,000 wanaweza kusherehekea.

https://p.dw.com/p/4ohzo
Ujerumani yajiandaa kuukaribisha mwaka mpya
Ujerumani yajiandaa kuukaribisha mwaka mpyaPicha: picture-alliance/A. Chown

Mwaka mpya wa 2025 utakaribishwa usiku wa leo na mabilioni ya watu kote ulimwenguni. Sherehe kubwa zaidi ya mkesha wa mwaka mpya nchini Ujerumani huenda ikafanyika tena mbele ya lango la Brandenburg mjini Berlin, ambapo, kulingana na waandaaji, hadi watu 65,000 wanaweza kusherehekea. Kulingana na mamlaka, maafisa wa polisi 3,000 watatawanywa mitaani usiku huko Berlin pekee.

Kwenye jimbo hili la North Rhine-Westphalia, NRW, zaidi ya maafisa wa polisi 7,300 wanahakikisha usalama. Hata kabla ya mwaka kuisha kulikuwa na operesheni nyingi za polisi kutokana na matumizi ya fataki mitaani.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Nancy Faeser alitangaza msako mkali wa vikosi vya usalama. Aliliambia shirika la habari la Ujerumani, dpa, kwamba wahalifu wanaoshambulia polisi na huduma za dharura lazima wahisi nguvu kamili ya sheria.