Ukraine yafunga mabomba ya gesi ya Urusi kwenda Ulaya
1 Januari 2025Moldova imetangaza hali ya hatari na Slovakia inatishia Kyiv kulipiza kisasi dhidi ya Kyiv. Chini ya mpango wa miaka mitano uliosainiwa mwaka wa 2019 Ukraine iliiruhusu Urusi kusafirisha gesi hadi Ulaya kupitia ardhi yake.
Lakini makubaliano hayo yanamalizika Januari mosi na Kyiv haina nia ya kuyarefusha kutokana na uvamizi wa Urusi. Mataifa kadhaa ya Ulaya mashariki bado yanaitegemea Moscow kwa mahitaji yao ya nishati. Hali ni mbaya sana nchini Moldova, ambayo inapakana na Ukraine na imelazimika kukabiliana na wanaharakati wanaotaka kujitenga ambao wanaungwa mkono na Urusi.
Nayo Slovakia imetishia kusitisha usambazaji wa umeme nchini Ukraine, hasa baada ya miundo mbinu ya nishati ya Kyiv kuharibiwa vibaya na karibu miaka mitatu ya mashambulizi ya Urusi.