1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya kutenga hifadhi ya wakimbizi

11 Machi 2016

Umoja wa ulaya una malengo ya kuandaa hifadhi ya waomba hifadhi kutoka Ugiriki katika miezi ijayo wakati huu ambapo mawaziri wake wakigubikwa na wasiwasi kuhusu uhalali wa kulazimisha wimbi la wahamiaji kurejea Uturuki

https://p.dw.com/p/1IBXB
Johanna Mikl-Leitner Thomas de Maiziere EU Innenministertreffen Brüssel
Mawaziri Johanna Mikl-Leitner na Thomas de MaizierePicha: picture-alliance/AP Photo/V.Mayo

Kamishna anehusika na suala la uhamiaji wa Umoja wa Ulaya Dimitris Avramopoulos aliwaambia waandishi habari kandoni mwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya ndani wa umoja wa ulaya kwamba mataifa mengine mwanachama wa umoja yanapaswa kupokea kiasi ya wakimbizi 6,000 kila mwezi, katika mpango ambao umefanikisha kupokelewa wakimbizi 900 tu hadi sasa.

Avramopoulos alibainisha jitihada za sasa za kugawanya idadi kubwa ya wakimbizi,imesababisha serikali za ulaya kutofautiana na baadhi ya serikali hizo kukataa kabisa mpango huo. Wengi wa kambizi hao wanatoka mataifa ya Syria na Iraq ingawa alisistiza kuwa jambo hilo lilikuwa la kihiyari katika ufanikishaji wake.

Wakimbizi wamekwama Uguriki

Kiasi ya wakimbizi 35,000 wamekwama nchini Ugiriki tangu Austria na mataifa yalio katika njia ya kuelekea Ujerumani yaanze kufunga mipaka, kwa lengo la kuwazuia kuwafuata wenzio zaidi ya milioni moja, ambao wamefanikiwa kufika katika maeneo ya ulaya ya kaskazini mwaka uliopita.

Griechenland Flüchtlinge an der Grenze zu Mazedonien bei Idomeni
Wakimbizi katika mpaka wa Idomeni UgirikiPicha: Reuters/S. Nenov

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ambae anakabiliwa na shinikizo la ndani lenye kugubikwa na chaguzi baada ya kufungua milango ya taifa lake kwa wakimbizi, aliyasistita mataifa ya Umoja wa Ulaya kugawana mzigo wa wakimbizi. Lakini machache yameonesha nia na wakosoaji wanasema hifadhi yoyote ya wakimbizi itakapowekwa itakuwa chini ya muongozo wa Ujerumani.

Wakimbizi 3,000 waondoka Ujerumani

Hapo jana Kansela Merkel wa alisema wahamiaji 3,000 wanarejea nchini Iraq kila mwezi na idadi hiyo inazidi kuongezka. Katika ufunguzi wa kampeni ya uchaguzi kwenye jimbo la Baden-Wuettemberg kiongozi huyo alisema baada ya kuishi kwenye mahema kwa muda mrefu na kuvunjwa moyo na mchakato wa kupata hifadhi nchini Ujerumani, wahamiaji hao wanaamua kurejea kwenye maeneo yaliyokombolewa kutoka mamlaka ya kundi la Dola la Kiislamu, IS.

Brüssel EU Gipfel - Angela Merkel
Kansela Angela Merkel wa UjerumaniPicha: Getty Images/AFP/E. Dunand

Lakini kwa upande wa mawaziri wa Umoja wa Ulaya kwa hivi sasa mjadala mkubwa ni kuhusu hitaji la kuandaa namna ya wakimbizi hao kubadili uelekeo au njia zikiwemo za kutumia bahari kwa Italia kutoka Albania au Libya. Idadi ya vifo kwa mwaka uliopita katika njia ya kuingia Italia kutoka Afrika ya Kaskazini, kwa kulingana na data za shirika la kimataifa la uhamiaji, inakaribia mtu mmoja kati ya 20, ikilianginshwa na chini ya mtu mmoja kati ya watu1,000 kwa wale wa Ugiriki na Uturuki.

Mwandishi: Sudi Mnette/DPA/RTR
Mhariri:Gakuba Daniel