1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wapitisha azimio la kusitishwa vita Gaza

12 Desemba 2024

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa wingi azimio la kutaka kusitishwa mara moja na bila masharti mapigano katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4o2dL
Ukumbi wa mikutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Ukumbi wa mikutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.Picha: Richard Drew/AP Photo/picture alliance

Wanachama 158 walipiga kura kuliunga mkono azimio hilo, tisa walilipinga na 13 walijizuia kupiga kura.

Azimio la kusitisha mapigano linachukuliwa kama ishara, kwani limekataliwa na Marekani na Israel.

Baraza hilo pia limeidhinisha azimio jengine linaloliunga mkono Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA.

Azimio hilo lilisikitishwa na sheria mpya ambayo inapiga marufuku shughuli za shirika hilo nchini Israel kuanzisa mwishoni mwa mwezi Januari.

Wakati huo huo, shirika la ulinzi wa kiraia la Gaza limeripoti kuwa mashambulizi ya anga ya Israel yamewaua watu wapatao 33, wakiwemo walinzi 12 wanaolinda malori ya misaada kwenye maeneo ya kusini mwa Mamlaka ya Palestina.