Umoja wa Ulaya kupeleka shehena ya silaha Ukraine
23 Machi 2023Matangazo
Kwa mujibu wa wanadiplomasia kadhaa wa ngazi za juu wa Umoja Ulaya, juma hili mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi wa umoja huo waliidhinisha mpango huo wa kuharakishwa utaratibu wa ununuzi mapema, ambapo viongozi wa mataifa hayo 27 wnatarajiwa kubariki hatua hiyo katika mkutano huu wa kilele ulianza leo.
Na Ukraine inakabiliwa na uhaba wa risasi baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa mapigano, mwezi uliopita Waziri Mkuu wa Estonia Kaja Kallas aliliwasilisha mezani wazo la Umoja wa Ulaya kuanzisha mpango wa ununuzi wa pamoja sawa na lile lililobuniwa wakati wa janga la UVIKO-19 katika kununua chanjo.