Umoja wa Ulaya na usawa wa jinsia
8 Machi 2006Usawa wa jinsia ni mojawapo ya malengo ya Umoja wa ulaya.Malengo hayo yametajwa ndani ya makubaliano ya Maastricht yaliyotiwa saini mwaka 1992.Kwa wakati mmoja na maadhimisho ya siku ya wakinamama ulimwenguni,kamisheni kuu ya Umoja wa ulaya imeitia njiani mikakati ya kuhimiza kushirikishwa kikamilifu wakinamama katika nchi zote 25 zanachama.
Katika umoja wa ulaya,wanawake wanalipwa asili mia 15 chini ya mishahara ya wenzao wa kiume kwa kazi ile ile.Kiwango cha wanawake wasiokua na ajira ni cha juu kuliko cha wanaume lakini wakinamama wanaishi miaka sita zaidi kuliko wanaume.Takriban thuluthi moja ya nyadhifa za juu katika mashirika na idara za serikali katika nchi za umoja wa ulaya zinadhibitiwa hivi sasa na wakinamama.Nchi inayoongoza upande huo ni Latvia ambako asili mia 44 ya wakinamama wanashikilia hatamu za uongozi.Inayoburura mkia ni Cyprus kwa asili mia 14.Hata Ujerumani haijapindukia kiwango cha asilio mia 30 kilichowekwa.
Ni nadra kuwaona wanawake wakikabidhiwa nyadhifa za juu-amesema mwenyekiti wa kamisheni kuu ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso katika warsha kuhusu usawa wa jinsia,inayoitishwa kila mwaka kuadhimisha siku ya wakinamama ulimwenguni.Mwenyekiti huyo wa kamisheni kuu ya Umoja wa ulaya anakiri:
“Katika sekta za kisiasa na kiuchumi bado wanawake hawawakilishwi vya kutosha.Hali hiyo ni sawa kuanzia Ulaya,Afrika na katika mabara mengi mengine.”
Binafsi katika kamisheni kuu ya umoja wa Ulaya inayoongoza nayeye mwenyewe Jose Manuel Barroso,madhamana wanapata tabu katika suala la usawa wa jinsia hasa katika tabaka za kati ambako idadi ya wanawake imefikia asili mia 25 tuu na sio 30 kama inavyoshauriwa ndani ya umoja wa ulaya.
Valerie Rampi ni msemaji wa idara ya waajiriwa ya kamisheni kuu.Anakiri kwamba kileleni hakauna wanawake wengi.
Na yeye pia anasema: "Kileleni mwa piramidi,kile tunachokiita ngazi ya juu ya uongozi ambayo ni sawa na wadhifa wa mkuu wa idara au katibu wa dola nchini Ujerumani,asili mia 16 tuu ya wanawake ndio wanaofanyakazi huko.”
Mpango wa kuwahimiza wakinamama na kuinua idadi yao katika tabaka za juu-utapelekea wanafanya kazi wakike wa umoja wa ulaya- ambao ni elfu kumi mia nane na 17 na wenzao wakiume 10.572,kuweza kupaanda daraja zote sawa na wenzao wa kiume.
Bibi Valerie Rampi anasema kamisheni kuu ya Umoja wa ulaya imejiwekea lengo la kuleta usawa wa jinsia katika daraja zote za jumuia hiyo.
Wafanyakazi wakike wa umoja wa ulaya wanajivunia fursa nzuri ya kulea watoto wao wakati wanaendelea na dhamana zao.
Hata hivyo idadi ya wakinamama wanaopigania kupanda vyeo imepungua,kinyume na ilivyotarajiwa kwasababu ya muda mrefu mtu anaobidi kufanya kazi kwa siku mjini Brussels.Madhamana wanatakiwa wafanye kazi kwa muda wa masaa 12 kwa siku.
Kamisheni kuu ya Umoja wa Ulaya imepanga kuunda tasasi ya kuchunguza masuala ya usawa wa jinsia katika nchi zanachama-Kitita cha euro milioni 50 kimetengwa kwaajili hiyo.Ingawa haijulikani bado taasisi hiyo itaongozwa na nani,lakini kila kitu kinaonyesha atakua mwanamke.