1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Ugaidi

UN yaanzisha siku ya kumbukumbu ya mauaji ya Srebrenica

DW Kiswahili | Iddi Ssessanga
Iddi Ssessanga
24 Mei 2024

Umoja wa Mataifa umeidhinisha azimio jana, linaloanzisha siku ya kila mwaka ya kukumbuka mauaji ya halaiki ya mwaka 1995 ya zaidi ya Waislamu 8,000 wa Bosnia, yaliofanywa na Waserbia wa Bosnia.

https://p.dw.com/p/4gDYe
Marekani New York 2024 | Kikao cha UN kuhusu Srebrenica | Kura
Matokeo ya kura kuhusu siku y kimataifa ya SrebrenicaPicha: Eduardo Munoz/REUTERS

Hatua hii imepingwa vikali na Waserbia wanaohofia kuwa itawafanya wote kuwa waungaji mkono wa mauaji ya halaiki. Kura hiyo katika Baraza Kuu ya Umoja wa Mataifa lenye jumla ya wanachama 193, imepita kwa kuungwa mkono na mataifa 84 dhidi ya 19 yaliopinga, huku mengine 68 yakijizuwia kupiga kura.

Soma piaUholanzi yaiomba radhi Srebrenica kwa mauaji

Azimio hilo linaitaja Julai 11 kama siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya mauaji ya halaiku ya Srebrenica, itakayoadhimishwa kila mwaka kuanzia miezi miwili ijayo.

Azimio hilo lililofadhiliwa na Ujerumani na Rwanda haliwataji moja kwa moja Waserbia kama wahusika wakuu wa mauaji hayo lakini lilipingwa vikali rais wa Bosniaya Serbia Milorad Dodik, na rais wa Serbia Aleksandar Vucic, aliejizungushia bendera ya Serbia akiwa ameketi barazani wakati wa kura.