MigogoroUlaya
Urusi na Ukraine zabadilishana mamia ya wafungwa wa kivita
31 Desemba 2024Matangazo
Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky amesema wafungwa 189 wa Ukraine, wakiwemo maafisa wa kijeshi, walinzi wa mpaka na walinzi wa kitaifa pamoja na raia wawili, wameachiwa. Ameushukuru Umoja wa Falme za Kiarabu kwa kufanikisha mabadilishano hayo.
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema askari 150 wa Urusi wameachiliwa huru kama sehemu ya ubadilishanaji huo ambao kila upande uliwaachia watu 150. Urusi na Ukraine zimefanya mabadilishano kadhaa ya aina hiyo ya wafungwa wakati wa vita vyao vya karibu miaka mitatu.
Kilichosababisha kutofautiana kwa idadi hiyo bado hakijawa wazi. Urusi imesema askari wake kwanza walipelekwa kwenye mpaka wa jirani yake Belarus, ambako walipewa msaada wa kisaikolojia na matibabu kabla ya kupelekwa Urusi.