1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yamfunga jela mwandishi habari wa Marekani Kurmasheva

23 Julai 2024

Mahakama nchini Urusi imemtia hatiani Alsu Kurmasheva, mwandishi wa habari wa Urusi mwenye uraia wa Marekani kwa kueneza habari za uongo kuhusu jeshi la Urusi na kumhukumu kifungo cha miaka sita na nusu jela.

https://p.dw.com/p/4ic36
Mwandishi habari - Alsu Kurmasheva
Kurmasheva alihukumiwa kwa kusambaza habari za uwongo kuhusiana na vita vinavyoendelea Ukraine.Picha: AP/picture alliance

Hukumu hiyo ilitolewa kwa Kurmasheva wakati wa kesi ya faragha iliyofanyika katika mji wa Kazan wa kusini magharibi mwa Urusi. Kurmasheva, ambaye ana umri wa miaka 47, aliifanyia kazi Radio Free Europe/Radio Liberty - RFE/RL, inayofadhiliwa na serikali ya Marekani.

Mahakama ya Urusi ilimtuhumu Kurmasheva kwa kusambaza habari za uwongo kuhusiana na ripoti zake za vita vinavyoendelea Ukraine. Rais wa RFE/RL Stephen Capus aliita kesi hiyo ya Urusi kuwa ni dhihaka kwa mkondo wa sheria. Kifungo cha mwandishi habari huyo mwanamke kinajiri siku chache tu baada ya mwandishi habari Mmarekani Evan Gershkovich kuhukumiwa kifungo cha miaka 16 jelanchini Urusi. Gershkovich, aliyelifanyia kazi jarida la Wall Street, alihukumiwa kwa mashitaka ya ujasusi. Marekani ilisema mashitaka hayo dhidi ya Gershkovich yalichochewa kisiasa na serikali ya Urusi.