Urusi yasema Assad ameondoka nchini Syria
8 Desemba 2024Katika taarifa yake, wizara hiyo haikusema alipo Assad lakini imesisitiza kuwa Urusi haikuhusika na mazungumzo ya kuondoka kwake.
Moscow ilikuwa na wasiwasi mkubwa juu ya matukio ya Syria na kuhimiza pande zote kujizuwia na vurugu na kusuluhisha masuala yote ya uongozi kupitia njia za kisiasa. Urusi imesema inawasiliana na makundi yote ya upinzani Syria kuhakikisha hilo linafanyika.
Waasi wa Syria watangaza marufuku ya kutembea nje usiku baada ya kuuangusha utawala wa Assad
Urusi pia imesema kambi zake za kijeshi Syria ziko katika tahadhari kubwa lakini hakuna kitisho dhidi yao kwa sasa.
Abu Mohammed al-Golani, kamanda wa zamani wa kundi la Qaida aliyekata mafungamano yake na kundi hilo miaka mingi iliyopita anaongoza kundi kubwa la waasi nchini Syria na anatarajiwa kuhusika kutoa muelekeo wa mustakabali wa taifa hilo.